Mbona nimeomba kwa muda mrefu ila sijajibiwa?

Swali: Baadhi ya watu wasiokuwa wasomi wanalalamika kwamba wamemuomba Allaah (´Azza wa Jall) miezi sita au mine au kwa muda mrefu lakini hata hivyo hawajaitikiwa. Je, waambiwe wafanye subira na pengine Allaah akawacheleweshea na kuwapa kilicho bora zaidi?

Jibu: Ndio, wafanye subira. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna muislamu yeyote anayeomba maombi ambayo ndani yake hamna dhambi wala kukata udugu isipokuwa Allaah atampa moja kati ya mambo matatu; ima atamcheleweshea maombi yake, akamcheleweshea nayo huko Aakhirah au akamwepusha na ovu sawa na mfano wake.” Wakasema: “Basi tufanye kwa wingi?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Allaah ni mwingi zaidi.”[1]

Allaah ni Mwingi wa hekima na mjuzi wa yote. Anaweza kumcheleweshea. Pengine kumjibu kukawa kuna madhara naye.

[1] Ahmad (03/18).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 58
  • Imechapishwa: 30/06/2019