Mwanamke ambaye ataposwa kwa yule mwanaume atakayemposa ni kama mwanamke wa kawaida wa sokoni. Si halali kwake kustarehe naye kwa kitu chochote. Hili linatupelekea katika kutaja jambo fulani; baadhi ya wanaume wanapomposa mwanamke wanazungumza naye kwenye simu maneno mengi. Hali imefikia kiasi cha kwamba nimefikiwa na khabari ya kwamba baadhi yao wanakesha usiku mzima na huku wanazungumza. Haya yametufikia. Hili ni jambo la haramu. Mwanamke huyu kwa hivi sasa ni mke wake au si mke wake? Si mke wake. Ni vipi ataweza kuzungumza naye na matamanio yake yasitikisike? Hili ni jambo gumu kuepukika. Baadhi ya watu wanasema kuwa wanazungumza naye ili kujua utamadukani alionao. Utapoishi naye ndipo utamjaribu. Ama kwa hivi sasa bado ni mwanamke ajinabi kwako. Yeye si halali kwako wala wewe si halali kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (46) hhttp://binothaimeen.net/content/1055
  • Imechapishwa: 11/03/2019