Maziwa, mafuta na nyama ya ng´ombe

1533- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maziwa yake ni shifaa, mafuta yake ni dawa na nyama yake ni maradhi.”

Bi maana ng´ombe.

Ameipokea al-Baghawiy katika “Hadiyth ´Aliy bin al-Ja´d”[1] kupitia kwa Zuhayr (bin Mu´aawiyah), kutoka kwa mke wake aliyesimulia ya kwamba alimsikia Maliykah bint ´Umar akipaka kiungo chake mafuta ya ng´ombe kilichokuwa kinamuuma na akasema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Maziwa yake ni shifaa, mafuta yake ni dawa na nyama yake ni maradhi.”

Cheni ya wapokezi wake ni nzuri – Allaah akitaka. Abu Daawuud ameipokea katika ”al-Maraasiyl”, at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr”, Ibn Mandah katika ”al-Ma´rifah” na Abu Nu´aym katika ”at-Twibb”. as-Sakhaawiy amesema katika ”al-Maqaaswid al-Hasanah”:

“Wanaume wake ni waaminifu. Lakini mwanamke aliyepokea kutoka kwa Maliykah hakutajwa kwa jina. Mpokezi aliyepokea kutoka kwa mwanamke huyo, Zuhayr bin Mu´aawiyah, amesema kwamba ni mwaminifu na kwamba ni mke wake. Abu Daawuud ameitaja kwenye “al-Maraasiyl” kwa sababu hakuwa na uhakika kama alikuwa ni Swahabah wa kike. Lakini hata hivyo wanachuoni wengi wamethibitisha kwamba alikuwa ni Swahabah. Hadiyth ina mapokezi yenye kuitolea ushahidi kutoka kwa Ibn Mas´uud ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jilazimieni na maziwa na mafuta ya ng´ombe na jiwekeni mbali na nyama yake. Kwani hakika maziwa na mafuta yake ni dawa na shifaa na nyama yake ni ugonjwa.”

Ameipokea al-Haakim ambaye alifanya wepesi katika usahihishwaji wake, kama nilivyolizungumza hilo kwa undani pindi nilipotaja njia zake zilizobaki katika baadhi ya majibu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwachinjia Udhhiyah wakeze ng´ombe katika mnasaba wa ´Iyd-ul-Adhwhaa´. Alifnaya hivo ima kwa sababu ya kubainisha kuwa ng´ombe inajuzu au kwa sababu alikosa kitu kingine cha kuchinja. Vinginevyo yeye kamwe hawezi kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala) kwa kitu kilicho na maradhi. al-Haliymiy amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilenga ukame wa al-Hijaaz. Huko nyama ya ng´ombe ni kavu na maziwa na mafuta yake ni yenye unyevunyevu. Ameona kuwa tafsiri hii ndio nzuri na Allaah ndiye anajua zaidi.”[2]

Hadiyth ya Ibn Mas´uud ni ushahidi wenye nguvu juu ya Hadiyth ilioko katika kichwa cha khabari.

[1] 1/122/11.

[2] 331.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (4/46-47)
  • Imechapishwa: 14/05/2019