Swali: Ni ipi hukumu ya kumzika maiti usiku?

Jibu: Inajuzu haja ikipelekea kufanya hivo. Yule mwanamke mweusi alizikwa usiku na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakujua jambo hilo. Hakuwakemea kwa sababu ya kumzika usiku isipokuwa kwa sababu hawakumjuza kuhusu kufa kwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwazika baadhi ya Maswahabah zake usiku na akayaangaza makaburi kwa mishumaa.

Swali: Inafaa kuwasha mataa makaburini kwa ajili ya kuzika usiku?

Jibu: Hakuna neno kuwasha mataa kwa sababu ni jambo la muda tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (15) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-24-11-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 21/09/2019