Muulizaji: Hasan Abu Shaqrah, mmoja katika walinganizi wa Salafiyyah Khaan Yuunus huko Palestina ambaye mayahudi walimfukuza nje ya nchi, alinipa khabari ya kwamba kabla hajafukuzwa alipata wito kutoka kwa mkurugenzi wa maeneo hayo ambaye alikuwa ni myahudi. Mkurugenzi yule akamweleza ya kwamba kuna watu waandamizi nchini waliomjia kwa kutaka kukutana na Hasan na anataka azungumze nao kikweli, ambapo akasema kuwa hakuna neno. Pindi Hasan alipoingia ndani ya chumba akaogopa na akawaona majenerali na mawaziri. Wakaanza kumuuliza kuhusu Salafiyyah, Da´wah mpya iliyojitokeza. Hasan anasema namna walivyokuwa wanaogopa kutaja neno “Salafiyyuun” na badala yake wanasema kuwa wanalingania katika matendo ya Maswahabah, kwa kuwa likithibitishwa neno hilo wanaingia jela. Mwishoni mwa mjadala mmoja wao akakasirika na kumwambia washikamane na Da´wah yoyote ile – kama Da´wah ya al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh – na walinganie kwayo, lakini Salafiyyah hii itayokuja kuwarudisha watu katika yale yaliyokuwa yakifuatwa na Abu Bakr na ´Umar – kwamba ni khatari. Ninaapa kwa Allaah namnukuu alisema hivi. Alisema kuwa hawatowaruhusu kuwaacha wamfuate Abu Bakr na ´Umar. Haya yalisemwa na jenerali mkubwa wa jeshi.

al-Albaaniy: Mwishowe mpaka makafiri wameona ukweli wa mambo. Kwa ajili hiyo mnatakiwa, nyinyi Salafiyyuun, kuwa na subira na kustahamili. Historia inajirudi. Twuubaa kwa wageni! Ni kina nani wageni?

“Twuubaa kwa wageni ambao wanarekebisha yale yaliyoharibishwa na watu katika Sunnah yangu!”[1]

[Katika upokezi mwingine imekuja:]

“Ni watu wachache kati ya watu wengi. Wenye kuwaasi ni wengi kuliko wale wenye kuwatii.”

Hivi sasa wameona wasifu zote mbili. Wamezipachika kwa al-Ikhwaan al-Muslimuun? Hapana. Wamezipachika kwa Hibz-ut-Tahriyr? Hapana. Wamezipachika kwa Jamaa´at-ut-Tabliygh? Hapana. Ni kama kondoo wasiojua ni wapi wanapoelekea.

[1] at-Tirmidhiy (2630) aliyesema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=2h99NHSwFU4
  • Imechapishwa: 19/11/2016