Swali: Imani ya mawalii ni kamilifu au kuna uwezekano wakawa na imani pungufu?

Jibu: Kuwa na imani kamilifu ni jambo gumu isipokuwa kwa Mitume (´alayhim-us-Swalaatu was-Salaam) na wale wafuasi wao waliowafikishwa na Allaah. Lakini hatumkatii yeyote kuwa na imani kamilifu. Isipokuwa tu Mitume (´alayhim-us-Swalaatu was-Salaam). Kuhusu wengine wana upungufu ima ukawa mwingi au mdogo. Hatumtakasi yeyote mbele ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 28/01/2017