Swali: Kuna mtu katika mji wetu hafungi wala haswali. Na nimemuona kwa macho yangu anacheza kamari. Na watu wake wanadai kuwa ni katika mawalii na watu walio karibu ya Allaah. Na kuna watu waaminifu wamenieleza ya kuwa anamtukana Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati nilipomkataza kitendo hichi kichafu, wakadai watu wake ya kuwa hii ni hali yake kwa uinje, ama kwa udani ni muumini. Ipi hukumu ya Kishari´ah kwa mfano wa huyu?

Jibu: Huyu ni mnafiki na wala sio muumini. Mfano wa watu kama hawa ni katika mawalii wa Shaytwaan. Mawalii wa Allaah ni wale wenye Imani na Taqwa. Anasema Allaah (Subhaanah):

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ

“Tanabahi! Hakika awliyaa wa Allaah (vipenzi Vyake wanaoamini Tawhiyd ya Allaah na kufuata amri Zake) hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika. Wale walioamini na wakawa wana taqwa (wanafuata amri za Allaah na Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). (10:62-63)

Namna hii ndivyo ilivyo katika Suurat Yuunus, hizi ndizo sifa za mawalii wa Allaah; ni wenye Imani na Taqwa kwa nje na kwa ndani. Na Akasema tena (´Azza wa Jalla):

وَمَا كَانُوا أَوْلِيَاءَهُ ۚ إِنْ أَوْلِيَاؤُهُ إِلَّا الْمُwتَّقُونَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

“Na hawakuwa walinzi (awliyaa) wake (Msikiti huo). Hawakuwa walinzi (awliyaa)wake isipokuwa wenye taqwa; lakini wengi wao hawajui.” (08:34)

Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Watu wa (… sauti haiko wazi… ) sio katika mawalii wangu, isipokuwa mawalii wangu ni waumini.” Mawalii wa Allaah na mawalii wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni waumini na watu wa Taqwa. Yule mwenye kujidhihirisha kwa kuacha Swalah, Swawm na anamtukana Allaah na Mtume Wake, huyu sio katika mawalii wa Allaah, bali ni katika mawalii wa Shaytwaan. Na ni wajibu aambiwe kutubu vinginevyo auawe, ni wajibu kwa mtawala wa Waislamu amwambie atubie la sivyo auawe. Kwa kuwa mwenye kuacha Swalah ni kafiri, aambiwe kutubu la sivyo auawe. Na mwenye kumtukana Allaah na Mtume wake, huyu anauawa hata bila ya kuambiwa kutubia kutokana na wanavyoona kundi katika wanachuoni. Muhimu ni kuwa, mtu huyu na watu mfano wake sio katika mawalii wa Allaah, isipokuwa ni katika mawalii wa Shaytwaan. Na wale wanaomtetea na kumhami na kusema kuwa kwa nje ni namna hii tu, lakini kwa ndani ni muumini, watu hawa ni katika jinsia yake nao ni mawalii wa Shaytwaan. Na ni watetezi wa shari na ufisadi. Baadhi ya Suufiyyah waliodanganywa ndio hufanya hivi. Ni wajibu kutanabahi kwa hili. Wanachuoni wa Sunnah (Rahimahumu Allaah) wamesema kwa yule mwenye kudai ni walii:

“Lau atatembea angani, akatembea juu ya maji, hazingatiwi kuwa ni katika mawalii wa Allaah mpaka matendo yake yatazamwe kwanza na kupimwa kwa mizani ya Kishari´ah.”

Akisimama katika mipaka ya Kishari´ah na kujulikana kuwa ni mwenye msimamo juu ya utiifu wa Allaah na Mtume Wake na kujiweka mbali na maharamisho ya Allaah na Mtume Wake, huyu ndiye muumini na walii. Na yakionekana kwake mambo ya ufasiki, kufanya ya haramu au kuacha ya wajibu, haya ni dalili tosha kuwa ni katika mawalii wa Shaytwaan na sio katika mawalii wa Allaah.” Kama alivyosema haya Imaam Shaafi´iy na Ahmad (Rahimahuma Allaah) na wasiokuwa wao katika wanachuoni. Muhimu ni kuwa, mfano wa watu kama hawa ni katika mawalii wa Shaytwaan. Na ni wajibu kwa mwenye kujua hilo kupeleka suala lake kwa kiongozi wa Waislamu mpaka ampe kinachomstahiki; amwambie kitubu la sivyo amuue.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 20/03/2018