Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na mavazi yenye picha za wanyama au watu?

Jibu: Haijuzu. Picha haijuzu. Kuvaa mavazi yaliyo na picha haijuzu, ni mamoja katika swalah na nje ya swalah. Haijuzu kubeba picha za viumbe wenye roho. Mtu akiswali nayo ni kubaya zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (56) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-12-30.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020