Swali: Karibuni makafiri watakuwa na sikukuu yao inayoitwa “Siku ya wapendanao”. Baadhi ya vijana wa Kiislamu wanatumia fursa ya kuvaa mavazi mekundu. Je, hii ni kasoro katika ´Aqiydah?

Jibu: Ndio. Haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayejifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Haijuzu kuafikiana nao pindi wanapokuwa na sikukuu zao na kuvaa mavazi ya sikukuu zao. Hilo halijuzu. Linawakweza hawa makafiri na ni aina ya ´ibaadah iliyozuliwa. Sikukuu hizi wamezizua kama Siku ya wapendanao, siku ya kuzaliwa na kadhalika. Wamezua sikukuu hizi. Allaah hajateremsha dalili yoyote juu ya hilo. Tusiwaige. Haitakiwi kamwe kuafikiana nao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.darulhadith.com/v2/roda-klader-infor-alla-hjartans-dag/
  • Imechapishwa: 14/02/2017