Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa vitambaa ambavyo vina michoro inayoashiria nyimbo na muziki? Je, inajuzu kuvivaa na kuswali navyo?

Jibu: Kila vazi ambalo lina ishara ya kitu cha haramu basi kulivaa itakuwa ni haramu. Vazi lililo na picha ni haramu. Vazi lililo na picha ya nyimbo na ala za muziki ni haramu. Vazi ambalo linalingania katika uzinzi ni haramu. Kwa sababu kama tunavosikia zipo nguo ambazo zinaandikwa maandishi mabaya mno. Mavazi haya pia ni haramu. Haifai kuyavaa. Mavazi yaliyo na picha ya mtu pia ni haramu na khaswa khaswa ikiwa ni picha ya kafiri au watu waovu. Katika hali hii uharamu unakuwa mkubwa. Lau sisi wananchi tungeshauriana kuzisusa bidhaa hizi zingelipotea. Lakini kwa masikitiko makubwa baadhi yetu wanawatetea wengine bila kuzingatia wala kufikiria.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1045
  • Imechapishwa: 05/03/2019