Mavazi ambayo anapaswa kuvaa mwanamke aliyefiwa na mume wake

Swali: Mwanamke ambaye amefiwa na mume wake, je avae mavazi meusi au haya ni maneno tu ya watu? Na je, atie wanja?

Jibu: Mwanamke ambaye amefiwa na mume wake, avae mavazi ambayo hayavutii watu kwake, sawa mavazi hayo yakiwa ni meupe au meusi. Akae eda miezi minne na siku kumi. Kama Alivyosema Allaah (Ta´ala):

وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا

“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, (hao wake) wangojee nafsi zao miezi minne na siku kumi (eda ya mfiwa).” (02:134)

Akae masiku haya naye yuko katika nyumba ya mume wake ambapo kafa ndani yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=651
  • Imechapishwa: 28/02/2018