Maulidi yamezushwa na Shiy´ah baada ya karne bora kwisha

Bid´ah ni nyingi. Watu wanazusha Bid´ah nyingi. Bid´ah haikubaliki na haitendewi kazi vovyote itakavyokuwa na pasina kujali aliyeifanya. Miongoni mwa Bid´ah ni yale yanayofanywa katika kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni Bid´ah. Haina dalili katika Qur-aan, Sunnah, uongofu wa Makhaliyfah waongofu na watu wa karne bora ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameshuhudia kuwa ni bora. Yamezushwa baada ya karne zote hizi pindi ujinga ulipoenea.

Watu wa kwanza waliozusha Maulidi ni Shiy´ah al-Faatwimiyyuun. Kisha wakayaiga wengineo ambao wanajinasibisha na Ahl-us-Sunnah kwa nia na malengo mazuri na wakadai kuwa ni katika kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sio katika kumpenda Mtume. Kupenda inakuwa kwa kufuata na sio kwa kuzusha:

Unamuasi Muumba na wewe unadai kuwa unampenda

Jambo hili katika kipimo ni fedheha!

Lau kama kweli mapenzi yako yangelikuwa ni ya kweli ungelimtii

Hakika mwenye kupenda kwa ampendae humtii.

Alama ya mapenzi ya kweli ni kwa kufuata. Ama kuzusha ni alama ya kuchukia. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitahadharisha juu ya Bid´ah na wewe unayahuisha na kuyazusha! Maana ya hilo ni kuwa unachukia Sunnah. Hivyo basi, ikiwa unachukia Sunnah ina maana kuwa unamchukia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa unataka kheri tubia kwa Allaah na jirudi. Ama ukaidai na jeuri, umeichagulia mabaya nafsi yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-it-Twahaawiyyah, uk. 175-176
  • Imechapishwa: 05/09/2020