Kutokana na tunavyojua tukirudi katika historia maulidi ya kwanza yalifanyika kwa jina la mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha kukafuatia kwa jina la mazazi ya ´Aliy bin Twaalib, kisha ya Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhumaa), kisha ya al-Hasan na al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa) halafu ya kiongozi aliyekuweko kipindi hicho. Sherehe sita. Haya yalitokea wakati gani? Wakati wa Faatwimiyyuun au sahihi zaiid ´Ubaydiyyuun. ´Ubaydiyyuun ni watu ambao walitaka kulinyanyua juu jambo lao na wakadai kwamba wao ni Faatwimiyyuun wakijinasibisha kwa Faatwimah az-Zahraa´ na wakataka kuthibitisha jina hili feki eti kwa kufungamana kwao na watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Matokeo yake wakawa wanasherehekea sherehe hizi sita kila mwaka kwa ajili eti ya kuwaadhimisha watu wa nyumbani kwa Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu wao uhalisia wa mambo ni kwamba si katika wao ndio maana wakajinasibisha na kutaka kuthibitisha ukoo huu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ajurry.com/home/%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%88%D9%84%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%88%D9%8A/
  • Imechapishwa: 04/11/2019