Maulidi ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu


Swali: Wapo watu wanaosema kwamba kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kumsomea Qur-aan maiti na mfano wa hayo ni miongoni mwa Bid´ah nzuri. Je, kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuna tofauti katika jambo hilo?

Jibu: Hapana. Hakuna Bid´ah yoyote ambayo ni nzuri. Bali Bid´ah zote ni upotevu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tahadharini kutokamana na mambo yaliyozuliwa.”

Kila (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akitoa Khutbah ya ijumaa akisema:

“Amma ba´d: Hakika maneno bora ni Kitabu cha Allaah. Uongofu bora ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Uovu wa mambo ni yale yaliyozuliwa. Kila kilichozuliwa ni Bid´ah. Kila Bid´ah ni upotevu. Kila upotevu ni Motoni.”

Kila Bid´ah ni upotevu. Kamwe hakuna Bid´ah nzuri. Bid´ah zote ni upotevu. Miongoni mwazo ni kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baadhi ya watu wanasherekea kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tarehe 12 Rabiy´ al-Awwaal. Hii ni Bid´ah. Kwa nini? Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusherehekea kuzaliwa kwake, Maswahabah hawakufanya hivo, wala Abu Bakr, wala ´Umar, wala ´Uthmaan, wala ´Aliy, wala karne ya kwanza, wala kane ya pili wala karne ya tatu. Usherehekeaji haukuzuka isipokuwa katika karne ya nne Hijriyyah ambayo yalizuliwa na ´Ubaydiyyuun waliokuwa wakiongoza Misri katika kane ya nne Hijriyyah. Walikuwa wakiwahukumu watu na walikuwa ni Shiy´ah waliochupa mipaka. Ndipo wakawaiga wakristo. Walipoona wakristo wanasherehekea mazazi ya al-Masiyh ndipo nao wakaanzisha kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo Bid´ah ya maulidi hakuisherehekea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah hawakuyasherehekea, wala karne ya kwanza, wala karne ya pili wala karne ya tatu. Karne zote bora hizi zilipita na hawajui kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka walipokuja ´Ubaydiyyuun ambao wanajiita Faatwimiyyuun wakidai kwamba ni katika kizazi ya Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa) – ilihali ni wakanamungu – wakazusha Bid´ah ya maulidi kwa sababu ya kuwaigiliza wakristo. Kwa hivyo hii ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Fr8zWiiI73c
  • Imechapishwa: 16/11/2019