Maudhui maalum kwa wanawake siku ya ´Iyd

Swali: Hivi sasa tunaona Khutbah mbili katika swalah ya ´Iyd. Khatwiyb anatoa Khtubah kisha anafanya Khutbah maalum kwa wanawake kwa maudhui mengine pamoja na kwamba kuna kipaza sauti. Ni ipi hukumu ya kufanya hivo?

Jibu: Inafaa kutokana na kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliwaelekezea wanawake maudhui yao kama ambavo aliwaelekezea wanawaume pia maudhui yao. Wanawake wana haki ya kufanyiwa maudhui maalum. Ikiwa sauti inawafikia basi Khatwiyb akawafanyie maneno yao maalum na awaeleze washikamane na maamrisho ya Allaah na wajisitiri kwa vazi la Hijaab. Yawe ni mazungumzo maalum kwa wanawake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 04/01/2019