Swali: Mwanamke hampendi mume wake na yeye mume anasema vivyo hivyo. Je, Shari´ah inamlazimu mume kumhudumikia na kuwahudumikia watoto wake baada ya kumpa talaka kwenye nyumba yao ya kujitegemea?

Jibu: Wakiachana wanapaswa kuelewana juu ya matumizi ya watoto. Mahakama itapeleleza hali yao. Wanatakiwa kupatana pamoja na walii wake mwanamke kuhusu matumizi kadhaa yanayotakiwa kila mwezi. Wasipoelewana basi suala hili litapelekwa mahakamani ndio yatayokadiria matumizi ambayo ni ya lazima. Lakini lililo bora zaidi kuliko hicho ni wao wenyewe kuelewana kuhusu matumizi munasibu juu ya watoto. Wasipoelewana basi walipeleke suala mahakamani. Hakuna mwingine zaidi ya mahakama wanaotakiwa kupeleleza suala hili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1283/%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%81%D9%82%D8%A9-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%88%D9%84%D8%A7%D8%AF-%D8%A8%D8%B9%D8%AF-%D8%B7%D9%84%D8%A7%D9%82-%D8%A7%D9%85%D9%87%D9%85
  • Imechapishwa: 28/12/2019