Matone baada ya kutwaharika na hedhi

Swali: Siku sita zilizopita nilitwaharika na ada ya mwezi. Baada ya hapo nikatokwa na matone ya damu baada ya kusafika mpaka wakati wa alasiri. Je, inafaa kuendelea kuswali na ´ibaada baada ya hapo?

Jibu: Ndio, haya si kitu. Matone baada ya kutwaharika hayazingatiwi kuwa ni hedhi. ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alifananisha kitu hicho na kutokwa na damu puani. Akasema mwanamke akitokwa na kitu kinachofanana kutokwa damu puani baada ya kutwaharika haidhuru.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1707
  • Imechapishwa: 15/04/2020