Swali: Kuna wanachuoni waliokuja nyuma ambao wanasema kwamba matendo ni sharti ya imani. Ni yepi makusudio ya maneno haya na ni sahihi?

Jibu: Si sahihi. Matendo ni katika imani. Imani ni kutamka kwa ulimi, kuamini moyoni na matendo ya viungo. Inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi. Hii ndio maana ya imani. Matendo yanaingia katika imani na sio sharti ya imani. Hakuna yeyote katika wanachuoni wanaozingatiwa aliyesema hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (85) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17635
  • Imechapishwa: 25/06/2018