Swali: Masuala ya kusema matendo ni sharti ya kusihi au sharti ya kukamilika kwa Imani ni masuala yaliyo na tofauti?

Jibu: Haya ni maneno batili. Haya ni maneno batili. Matendo ni katika Imani na sio sharti na wala hayaikamilishi Imani. Matendo ni katika Imani. Hakuna Imani pasina matendo na wala hakuna matendo pasina Imani. Kama jinsi hayasihi matendo pasina Imani, kadhalika haisihi Imani pasina matendo. Acheni falsafa hizi za kusema ni sharti ya kutimia, sharti ya kusihi na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (63) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13810
  • Imechapishwa: 16/11/2014