Matangamano ya mwanamke na washemeji


Swali: Ni ipi hukumu ya mtu  kuingia nyumbani kwa kaka yake na kuchanganyikana na mke wa kaka yake kwa idhini ya kaka yake na mke wake anaacha uso wazi?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Haya ni maovu. Anatakiwa kumwamrisha kufunika uso wake:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabanati zako na wanawake wa waumini wajiteremshie jilbaab zao. Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane wasiudhiwe. Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (33:59)

Bi maana wafunike nyuso zao kwa ncha ya jilbaal zao.  Jilbaab ni vazi kubwa, kama vile ´Abaa´ah. Mbele ya wanaume ambao sio Mahram zake anatakiwa kufunika uso wake kwa ncha ya jilbaab yake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema vilevile:

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ

“Mnapowauliza wake zake haja, basi waulizeni nyuma ya pazia.” (33:53)

Bi maana nyuma ya nyuso zilizofunikwa kwa mavazi, kuta, mlango au kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (85) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17635
  • Imechapishwa: 14/10/2018