Swali: Vipi tutaamiliane na ndugu ambao wanafanyia mzaha Sunnah?

Jibu: Tangamana nao kama ulivyosikia; kwa kuwanasihi na kuwakataza. Wasiponyooka jitenge nao. Kwa kuwa mwenye kufanyia mzaha Sunnah ni kafiri – na tunaomba kinga kwa Allaah. Ni kafiri. Mwenye kufanyia mzaha na maskhara Sunnah ni kama mfano wa mwenye kufanyia maskhara Qur-aan. Ni sawa sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14005
  • Imechapishwa: 19/04/2018