Matamshi mabaya ikiwa mtu nia yake ni nzuri

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa kusahihisha matamshi si jambo muhimu muda wa kuwa moyo umesalimika?

Jibu: Ikiwa anakusudia kuyapitisha matamshi katika lugha ya kiarabu ni sahihi. Sio kitu muhimu kwa upande wa kusalimika kwa ´Aqiydah matamshi yakawa hayapitiki katika lugha ya kiarabu muda wa kuwa ile maana imefahamika na kusalimika. Lakini ikiwa anakusudia kusahihisha matamshi yanayofahamisha ukafiri na shirki, basi maneno yake si sahihi. Bali ni muhimu kuyasahihisha. Hatuwezi kumwambia mtu aseme atakacho muda kuwa nia yake ni sahihi. Bali tunatakiwa kusema maneno yaliyofungamana kwa yale yaliyoletwa na Shari´ah ya Kiislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Manaahiy al-Lafdhwiyyah, uk. 03
  • Imechapishwa: 01/07/2022