Swali: Nia ya kufunga siku moja inatosheleza juu ya kufunga siku zengine zote?

Jibu: Ni jambo linalojulikana kwamba kila mtu anayeamka mwishoni mwa usiku kula daku amekusudia kufunga siku hiyo. Kwani kila mwenye akili hufanya mambo kwa kutaka kwake mwenyewe. Hafanyi kitu pasi na kutaka kwake mwenyewe. Yale matakwa ndio nia yenyewe. Mtu hali mwishoni mwa usiku isipokuwa ni kwa sababu amenuia funga. Kama ingelikuwa kula tu basi isingelikuwa ni katika mazowea yake kukusudia kula katika kipindi hichi. Hii ndio nia yenyewe. Lakini swali hili linahitajika iwapo tutakadiria kama kuna mtu amelala kabla ya kuzama kwa jua Ramadhaan na akabaki amelala na asiamshwe na yeyote mpaka ikaingia alfajiri ya siku ya pili, huyu hakunuia kufunga kwa ajili ya siku ya kufuata. Je, swawm yake ni sahihi kutokana na nia yake iliyotangulia, au swawm yake si sahihi kwa sababu hakunuia wakati wa usiku wake? Funga yake ni sahihi. Maoni yenye nguvu ni kwamba inatosha kuweka nia kwa ajili ya kufunga Ramadhaan mwanzoni mwa Ramadhaan na hakuna haja ya kufanya nia upya kila siku. Isipokuwa kama kumepatikana sababu inayomjuzishia mtu kufungua ambapo akafungua katikati ya mwezi; huyu ndiye anahitajia kuweka nia mpya kwa ajili ya kufunga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/176-177)
  • Imechapishwa: 05/05/2021