Swali: Kabla ya mimi kuja katika nchi hii iliobarikiwa nilitahadharishwa juu ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, as-Suhaymiy, al-´Abbaad na Amaan, bi maana Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy.

Jibu: Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy wameshafariki. Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (kafariki 1206) kabla ya takriban ya miaka 250. Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy alifariki mwaka wa 1416. Allaah amrehemu rehema kunjufu. al-´Abbaad ni Shaykh ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad; Shaykh wetu na Shaykh wa Madiynah nzima katika Hadiyth na elimu nyenginezo. Allaah amuhifadhi. Bado yuhai na anafunza ndani ya msikiti huu. Tahadhari hii kutoka kwa masikini hawa inajulisha juu ya ujinga wao na kuwa kwao mbali na dini ya haki. Wamekufanya nini hawa uliowataja mpaka utahadharishe nao? Kubwa walilonalo ni kwamba wamelingania katika Tawhiyd na kutahadharisha shirki. Hichi ndicho wanachofanya. Haya ndio yamepelekea wewe kutahadharisha nao? Kuwa makini. Watu hawa ni wapotofu. Ambao wanakutahadharisheni juu ya wanachuoni ni wapotofu na wanachotaka ni nyinyi mbaki juu ya shirki wanayokulinganieni kwayo; kuyaabudia makaburi, kuwaomba uombezi wafu waliyomo ndani ya makaburi, kuwalekea wafu waliyomo ndani ya makaburi na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=ZzYfkpmN4TQ
  • Imechapishwa: 15/01/2021