Matabano yanatakiwa kuwa kitendo cha mtu kujitolea

Swali:  Ni ipi hukumu ya kufungua kituo cha matabano baada ya kupata idhini ya wanachuoni?

Jibu: Vituo kama hivi visifunguliwe. Watu watavitumia kwa ajili ya kula mali za watu. Kusifunguliwe vituo kwa ajili ya matabano. Matabano ni kitendo ambacho mtu hujitolea. Akipewa kitu kwa ajili ya matabano yake, akipokee. Lakini hata hivyo asiwawekee watu sharti ya kiwango cha pesa kadhaa na kufunga duka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (60) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16548
  • Imechapishwa: 16/09/2017