Maswali magumu kwa Ahmad al-Khaliyliy


Tusome yaliyotajwa katika Suurah “Twaahaa” ambapo Allaah alimzungumzisha Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah anasema hali ya kuwa akimzungumzisha Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَهَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ إِذْ رَأَىٰ نَارًا فَقَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِقَبَسٍ أَوْ أَجِدُ عَلَى النَّارِ هُدًى فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَىٰ إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي

“Na je, imekufikia hadithi ya Muusa? Alipouona moto akawaambia ahli zake: “Bakieni hapa, hakika nimeona moto, huenda nikakuleteeni kutoka humo kijinga cha moto au nipate kwenye huo moto mwongozo. Basi alipoufikia, aliitwa: “Ee Muusa! Hakika Mimi ni Mola wako, hivyo basi vua viatu vyako, kwani hakika wewe uko katika bonde takatifu la Twuwaa. Nami nimekuchagua, basi sikiliza yanayofunuliwa Wahy: Hakika mimi ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, hivyo basi niabudu na simamisha swalah kwa ajili ya kunitaja.”[1]

Ni kutoka kwa nani Muusa aliisikia sauti hii inayotoka sehemu patupu – kama al-Khaliyliy anavyodai? Muusa alimsikia nani akisema:

إِنِّي أَنَا رَبُّكَ

“Hakika Mimi ni Mola wako?”

Ni nani aliyesema:

وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَىٰ إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي

“Nami nimekuchagua, basi sikiliza yanayofunuliwa Wahy: Hakika mimi ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, hivyo basi niabudu?”

Aliyasikia kutoka sehemu patupu? Hii sehemu patupu ndio iliyodai kuwa ni mola wa Muusa na pakamuomba Muusa kumuabudu? Hakika huu ndio upotevu wa wazi kabisa na ni kuyapotosha maneno ya Allaah, Mola wa walimwengu. Hivi kweli kuna mtu mwenye busara anaweza kuamini kitu kama hicho?

[1] 20:09-14

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 235
  • Imechapishwa: 15/04/2017