394- Nilimsikia mtu mmoja akimuuliza Ahmad: “Ninapofika katika swalah ya ijumaa, basi inatokea kwamba nakaa njiani mara nyingi. Hilo linapelekea kwamba nashindwa kuhudhuria swalah ya mkusanyiko kwa muda wa siku mbili. Je, naruhusiwa kuacha kuswali swalah ya ijumaa?” Akasema: “Sijui. Swalah ya ijumaa ina fadhilah zake na kadhalika swalah ya mkusanyiko.”

395- Nilimsikia Ahamd akiulizwa kama swalah ya ijumaa inamuwajibikia msafiri. Akajibu:

“Hapana.”

396- Nilimsikia Ahmad akiulizwa kuhusu imamu ambaye ni Jahmiyyah amewaongoza watu katika swalah ya ijumaa. Je, swalah hiyo ya ijumaa irudiliwe kabla au baada? Akajibu:

“Baada ya swalah ya ijumaa.”

402- Nilimsikia Ahmad akiulizwa kuhusu imamu mjinga ambaye hakutoa Khutbah kabla ya swalah ya ijumaa. Akasema:

“Aswali Rak´ah nne.”

403-  Nilimsikia Ahmad akisema:

“Mtu akijiunga katika swalah ya ijumaa wakati wamekaa katika Tashahhud, basi anatakiwa kuswali Rak´ah nne.”

408- Nilimuona Ahmad anakuja katika swalah ya ijumaaa punde kidogo kabla ya jua kupindukia.

409- Nilimsikia Ahmad akiulizwa kuhusu mtu ambaye amepitikiwa na usingizi siku ya ijumaa wakati imamu anatoa Khutbah. Akasema:

“Anatakiwa kubadilisha nafasi ili usingizi umwondoke.”

415- Nilimsikia Ahmad akiulizwa kuhusu mtu ambaye anaswali swalah ya ijumaa nje ya msikiti na milango ya misikiti imefungwa. Akasema:

“Nataraji hakuna neno.”

417- Nilimsikia Ahmad akisema:

“Mtu akiswali Rak´ah nne baada ya swalah ya ijumaa, ni sawa. Akiswali Rak´ah mbili baada ya swalah ya ijumaa, ni sawa. Akiswali Rak´ah sita baada ya swalah ya ijumaa, ni sawa.”

420- Nilimuuliza Ahmad ni kipi msafiri anatakiwa kufanya akijiunga na swalah ya ijuma wakati imamu amekaa katika Tashahhud. Akasema:

“Aswali Rak´ah nne.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 82-86
  • Imechapishwa: 05/07/2019