Masomo yanayotofautiana na fatwa za Ibn Baaz na Ibn ´Uthaymiyn

Swali: Baadhi ya waalimu zetu madrasah katika somo la Fiqh wameshauri kusoma Fiqh katika moja ya madhehebu ya ki-Fiqh. Lakini hata hivyo tunapata baadhi ya mambo yanaenda kinyume na Fataawaa za wanachuoni kama mfano wa Shaykh Ibn Baaz na Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahumaa Allaah). Tufanye nini; tutangulize yaliyo kwenye madhehebu au yaliyo kwenye fatwa?

Jibu: Kusoma sio utendaji kazi. Wewe soma Fiqh kama jinsi ilivyo. Ama inapokuja katika utendaji kazi unatakiwa kuchukua ile kauli ilio na nguvu. Tendea kazi ile kauli ilio na nguvu. Hapa ni pale ambapo uko na uwezo wa kuona ni kauli ipi ilio na nguvu. Ikiwa huna uwezo wa kufanya hivo waulize wanachuoni. Wewe hivi sasa soma Fiqh katika moja ya madhehebu mane. Lakini usijibu na kutenda kazi kwa mujibu wa madhehebu hayo isipokuwa baada ya kuhakikisha dalili na mashiko yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13965
  • Imechapishwa: 11/04/2018