Masomo sio udhuru wa kuchelewesha swalah

Swali: Mimi ni mwanafunzi ninayesoma katika chuo kikuu. Baadhi ya nyakati napitwi na swalah ya Dhuhr kutokana na ile Sunnah iliyomo ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, inajuzu kuswali swalah ya Dhuhr pamoja na swalah ya ´Aswr na bila ya kuswali Sunnah ya Dhuhr au niswali swalah ya Dhuhr pamoja na ´Aswr zote kwa pamoja?

Jibu: Haijuzu kwako kukusanya. Ni wajibu kwako kuswali Dhuhr kwa wakati wake. Haifai kwako kuichelewesha mpaka wakati wa ´Aswr. Masomo sio udhuru juu ya hilo. Bali ni wajibu kwako kuswali Dhuhr kwa wakati wake. Imewekwa katika Shari´ah kwako kutekeleza Sunnah; ni Rakaa´ nne kabla ya Dhuhr na Rakaa´ mbili baada yake, kama alivyokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Swali Rakaa´ nne kabla ya Dhuhr na mbili baada yake. Hizi ni Sunnah. Kilicho muhimu zaidi ni faradhi. Ni wajibu kwako kuswali faradhi kwa wakati wake. Nazo ni Rakaa´ nne kwa yule ambaye ni mwenyeji na Rakaa´ mbili kwa yule ambaye ni msafiri, kama ambavyo inatambulika. Haifai kwako kuichelewesha mpaka ´Aswr ilihali wewe ni mwenyeji. Lakini kwa ambaye ni msafiri hakuna neno kufanya hivo. Kadhalika mgonjwa. Ama kutumia hoja ya masomo hapana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziy bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=1241&PageNo=1&BookID=5
  • Imechapishwa: 12/03/2018