Swali: Ni bora kwa mwanafunzi kuoa au aendelee kutafuta elimu? Nimesoma kuwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) aliacha kuoa na akaendelea kutafuta elimu?

Jibu: Ikiwa anachelea juu ya nafsi yake kutumbukia katika madhambi, itakuwa ni wajibu kwake kuoa. Hili halizuii kutafuta elimu. Lakini ikiwa hachelei juu ya nafsi yake kutumbukia katika madhambi, basi aendelee kutafuta elimu na pindi atapomaliza ndio aoe. Inategemea na hali yenyewe ya mtu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (59) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-29-01-1438_0.mp3
  • Imechapishwa: 03/11/2017