Endapo mtu atafanya maskhara na Siwaak na kwa mfano akasema “ni Siwaak zipi hizi mnazoweka mifukoni mwenu” ilihali hii leo watu wanatumia miswaki ya kisasa na dawa ya meno – mambo gani mnatuletea haya? Huyu ni kafiri. Kwa sababu amefanya istihzai na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwenye kufanya maskhara na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefanya maskhara na Mtume. Mwenye kufanya maskhara na Mtume amefanya maskhara na Allaah na hivyo ni kafiri.

Mambo yanayoharibu Uislamu wa mtu ni lazima watu wayatambue na khaswa hii leo. Uislamu una vichenguzi vyake kama ambavyo wudhuu´ una vichenguzi vyake. Ni lazima kwa waislamu hii leo, pamoja na fitina iliojaa, maswali mengi, kuropoka kwa wingi, ujasiri wa kipumbavu kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mtu anaweza kutumbukia katika ukafiri pasi na yeye kujua. Kwa ajili hiyo nasaha zangu kwa waislamu wasome vichenguzi vya Uislamu kama wanavosoma vichenguzi vya wudhuu´.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qawl-ul-Mustajaadu fiy Mujaazafaat-id-Haddaad https://ia800202.us.archive.org/4/items/Mouhadaraat-ElJami/Amaan-ElJami28.mp3
  • Imechapishwa: 29/02/2020