Mashaytwaan hawawasogelei watu wema katika Ramadhaan

Miongoni mwa mambo maalum ya Ramadhaan ni kuwa milango ya Pepo hufunguliwa kwa matendo mema. Wale wanaofanya matendo mema wanaingia milango hii. Kila mmoja anaingia kupitia mlango unaoafikiana na matendo yake. Wale wenye kufunga wana mlango wao. Wale wenye kusimama usiku wana mlango wao. Wale wanaotoka kwenda kupigana Jihaad wana mlango wao na kadhalika. Milango hii hufunguliwa kwa watu wa kheri wenye kumtii Allaah.

Hali kadhalika milango ya Motoni hufungwa kwa waumini. Maasi hupungua katika mwezi huu. Matendo mema huwa mengi. Mashaytwaan hufungwa minyororo ili wasiwafikie watu wema. Ama kuhusiana na waovu, huvamiwa na Mashaytwaan sawa katika Ramadhaan na nje yake. Ni katika uhusiano wa watu wema ndio wanafungwa minyororo ili wasiwaharibie matendo yao. Ni katika fadhila za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ya kwamba Anawasitishia adui yao ambaye alikuwa akiwashughulisha mwaka mzima. Wakati Ramadhaan inapoingia hufungwa ili wasiwafikie watu wema ili waweze kutenda matendo mema na kusalimika na adui yao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kunadi hunadi: “Wewe mwenye kukimbilia kheri! Njoo! Wewe mwenye kukimbilia shari! Soma!”

Huu ni wito kutoka kwa Allaah kwenda kwa yule Anayemtaka katika waja Wake. Huu ni mwezi mkubwa na msimu mtukufu na kheri nyingi kwa yule Aliyewafikishwa na Allaah na Akamdirikisha nao, akafunga michana yake, akasimama masiku yake na akautumia wakati wake vizuri. Ramadhaan ni mwezi wenye baraka kwa njia zote. Hakuna dakika hata moja ndani yake isipokuwa ni kheri kwa yule muumini Aliyewafikishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/%2015248
  • Imechapishwa: 19/05/2020