Mashaykh wa mseto wanaonyamazia shirki na Bid´ah


Swali: Baadhi ya wanachuoni wa leo wanasema kuwa mtu hakufuru akisema au akifanya jambo la kufuru mpaka akusudie kwa moyo. Ni yepi maoni yako?

Jibu: Hili ni kosa. Mtu anakufuru kwa moyo, kwa mdomo na kwa matendo. Isipokuwa atapotenzwa nguvu na wakati huohuo moyo wake ukatua juu ya imani. Akitenzwa nguvu kwa kupigwa, kutishiwa kuuawa kama alivofanywa ´Ammaar, Ibn Mas´uud na wengineo ambapo wakaafikiana nao na Mtume (Swalla Alalahu ´alayhi wa sallam) akawakubalia jambo hilo. Lakini moyo unapaswa kutua juu ya imani na kumwabudu Allaah (Ta´ala) pekee.

Swali: Wanachuoni hawa wanahudhuria sherehe hizi na wanazitia baraka na wao ndio wanakuwa viongozi?

Jibu: Ikiwa wanafanya pamoja nao shirki basi ni washirikina. Ikiwa sherehe hizo zina shirki na wanafanya pamoja nao shirki basi ni washirikina. Ama ikiwa sherehe hizo ni kula na kunywa na ndani yake hakuna shirki sio washirikina. Ama ikiwa ni sherehe za kumtukana Allaah, Mtume, kuwaomba au kuwataka msaada wafu na wao na wanaona kuwa hakuna neno kushirikiana nao wakashirikiana pamoja nao wamemkufuru Allaah na wamekufuru.

Swali: Wakati mwingine anaweza kuhudhuria ili ajue kile wanachokifanya ili aweze kuyazungumzia?

Jibu: Hili ni lazima kwake. Iwapo atahudhuria kwa ajili ya kukemea maovu basi ni mwenye kulipwa thawabu. Ni kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akihudhuria hajj ili kuongea nao na akizunguka Minaa na akiwaambia: “Enyi watu wangu! Mcheni Allaah na mwabuduni Allaah pekee.”

Akiwazungukia sehemu zao Minaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 133-134
  • Imechapishwa: 11/09/2019