Masharubu yanapunguzwa na hayanyolewi

Swali: Bora ni kuyanyoa masharubu au kuyapunguza?

Jibu: Bora ni kuyapunguza masharubu. Hivyo ndivyo ilivyokuja katika Sunnah; ima mtu anatakiwa kupunguza ncha zake zinazofuata ili midomo yake ionekane au azipunguze zote ili yabaki madogo kabisa.

Ama kuzinyoa sio katika Sunnah. Baadhi ya watu wanasema kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa kutumia kipimo juu ya kunyoa kichwa katika hajj na kupingana na andiko hayawazingatiwi. Kwa ajili hii amesema Maalik kuhusu kunyoa:

“Ni Bid´ah iliyoletwa na watu. Haitakiwi kuacha yale yaliyoletwa na Sunnah. Kwani kuifuata ni uongofu, wema, furaha na mafanikio.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/129)
  • Imechapishwa: 30/06/2017