Masharti ya ndoa ili iwe sahihi Kishari´ah


Swali: Kuna mtu kampa binti yake mtu mwengine na walikuwa wakiongea katika kikao bila ya ndoa ya rasmi, na binti huyo ana miaka kumi. Na baada ya kupita miaka miwili mambo yakabadilika na binti akaolewa na mtoto wa mtu yule aliyempa binti yake. Ipi hukumu ya hili?

Jibu: Jambo la kwanza ikiwa ni kwa ridhaa ya binti na kuna mashahidi wawili ndoa imetimia. Na ikiwa binti hakuridhia au hakuna mashahidi wawili, ndoa haisihi. Kwa kuwa lililo la wajibu ni kumshauri binti anapofikisha miaka tisa. Haijuzu kumuoza ila kwa idhini yake, na kuridhia kwake ni pale unapomuona kimya. Ikiwa baba yake alipomuoza hakumshauri au alifanya hivyo lakini hapakuwepo mashahidi wawili, ndoa hii siyo sahihi. Ama kama alimshauri na akaridhia kwa kukaa kwake kimya au kwa kuongea na kukahudhuria mashahidi wawili, sahihi ni kuwa ndoa imepita. Na sio katika sharti kumuuliza “Umekubali kumuoa”. Bali yatosha [walii wa mwanamke] akisema nimekuoza binti yangu, imepita kukitimia sharti zingine na kukawa hakuna vikwazo.

Swali: Lakini katika hali hii ni kuwa baada ya miaka miwili aliolewa na mtoto wa yule aliyekuwa amempata binti yake.

Jibu: Ikiwa ndoa ile ya kwanza ilipita, ndoa hii ya pili ni batili. Na ikiwa ndoa ile ya kwanza haikupita, ndoa hii ya pili ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid= 8177
  • Imechapishwa: 10/04/2022