Swali 128: Ni yepi masharti ya Jihaad? Je, ni yenye kutimia hii leo?

Jibu: Masharti ya Jihaad yanatambulika:

1- Waislamu wawe na nguvu ambazo kwazo wataweza kupambana na makafiri. Wawe na nguvu na uwezo ambao kwao wataweza kupambana na makafiri. Ni lazima kupatikane jambo hili. Ama wakiwa hawana uwezo na hawana nguvu, basi hakuna Jihaad yenye kuwalazimu. Mtume na Maswahabah walikuwa Makkah kabla ya kuhajiri. Hawakuwekewa Shari´ah ya Jihaad kwa sababu hakuwa na uwezo.

2- Jengine ni lazima Jihaad iwe chini ya uongozi wa Kiislamu na kwa amri ya mtawala. Kwa sababu ni jukumu linalomwangalia mtawala wa waislamu mtawala. Yeye ndiye mwenye kuiamrisha, kuipanga, kuisimamia na kuiendesha. Ni jukumu linalomwangalia mtawala. Sio jukumu linalomwangalia kila mmoja, kila kundi likaenda au likapambana bila idhini ya mtawala.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 308
  • Imechapishwa: 24/11/2019