Masharti tano ya kufanya uasi kwa mtawala


Swali: Je, haijuzu kufanya uasi kwa mtawala hata kama atakuwa hahukumu kwa aliyoteremsha Allaah?

Jibu: Tumeshasema mara nyingi kuwa haijuzu kufanya uasi kwa mtawala isipokuwa kwa masharti matano:

1- Afanye kufuru na isiwe dhambi kubwa au maasi.

2- Kufuru iwe ya wazi na haina utata.

3- Kuwe dalili ya hilo kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… isipokuwa ikiwa ni kwa kufuru ya wazi ambayo mna dalili juu yake kutoka kwa Allaah.”

4- Awepo badali atayechukua nafasi yake ambaye atahukumu kwa Shari´ah.

5- Kuwepo na uwezekano [wa kumuondosha pasi na kupatikana madhara].

Inajuzu ikiwa kutapatikana masharti haya matano. Vinginevyo [ni lazima] kuwa na subira na ushirikiano na wengine ikiwa ni pamoja na mtawala katika kumtii Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://shrajhi.com//Live/ArID/1893
  • Imechapishwa: 05/09/2020