Mfano wa mashairi yenye kuchupa mipaka ni yale yaliyokuja katika Qaswiydah ya “al-Burdah” al-Buswayriy akimzungumzisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kusema:

Hakika katika ukarimu wako ni pamoja na dunia na Aakhirah

 na miongoni mwa elimu yako ni elimu ya Ubao na kalamu

Hapana shaka kwamba hii ni shirki. Bali ni katika shirki kubwa tusiposema kuwa amemfanyia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sifa ambazo ni maalum kwa Mola na akampokonya nazo.

Ikiwa miongoni mwa ukarimu wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni pamoja na dunia na Aakhirah, basi hapakubaki chochote kwa ajili ya Allaah (Ta´ala). Ikiwa miongoni mwa elimu yake – yaani baadhi ya elimu anayoijua – ni pamoja na elimu ya Ubao na elimu, hapakubaki elimu yoyote kwa ajili ya Allaah. Mfano wa maneno kama haya yanayofikia kwenye kiwango hichi au chini yake ni mambo yasiyofaa kwa muislamu kuyasema juu ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hivyo haifai kwa yeyote kuyatamka. Ni mamoja kwa njia ya mashairi au ya kawaida.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (09) http://binothaimeen.net/content/6738
  • Imechapishwa: 21/11/2020