Mashaa´ Allaah Kwenye Kio Cha Gari

Swali: Mwenye kuweka neno “Allaah alivyotaka” –ما شاء الله – kwenye gari yake kama kinga dhidi ya kijicho akatazwe?

Jibu: Ndio. Ni hirizi. Akiiweka kutokana na khofu ya kijicho ni hirizi. Hali kadhalika kama kungelikuwa kitu kingine cha Qur-aan.

Swali: Na vipi kuweka Qur-aan sehemu ya mbele ya gari…

Jibu: Ni hirizi pia. Haijuzu kuitumia Qur-aan kama hirizi. Ama kuwa na Qur-aan kwa ajili ya kusoma ndani yake ni vizuri. Hata hivyo haijuzu kuamini kuwa Qur-aan inakinga kijicho. Ni nia moja wapo ya kutumia hirizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20%20-%2025%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017