Swali: Kipindi cha mwisho Salafiyyah na walinganizi wake wamekuwa ni wenye kushambuliwa sana na kutukanwa. Wamehusishwa na tuhuma za ugaidi na makundi ya kigaidi. Ni vipi kutaraddiwa tuhuma hizi?

Jibu: Hivi ndivo wafanyavyo wanafiki katika kila zama. Wanautuhumu Uislamu kwa mambo yasiyoendana na Uislamu kwa lengo la kuuchafua machoni mwa watu. Hili si geni kabisa. Hapo kabla walikuwa wakiona kuwa Mitume ndio wenye kuleta mikosi. Waliwalaumu Mitume kutokana na masaibu iliokuwa ikiwapata. Yote haya ni katika mambo ya kipindi kabla ya kuja Uislamu na haijuzu. Wanazuoni na watu wema wanainufaisha jamii. Wanaboresha na kusalimisha jamii. Ni kwa nini hamuwatuhumu majanga hayo watenda madhambi? Hivo ndivo ilivyo kweli. Ama kuwatuhumu masaibu hayo watu wema ni katika kuamini mikosi ambayo nyumati zilikuwa zikiwatuhumu Mitume.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 12/03/2022