Swali: Ni marejeo yetu unayotupendezea kujua mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Kila kitabu cha ´Aqiydah ambacho kimeandikwa na maimamu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kinaelezea mfumo huu. Vitabu hivyo vinaitwa vitabu vya imani, vitabu vya Tawhiyd, vitabu vya ´Aqiydah, vitabu vya Sunnah. Ni tungo nyingi. Kinachonidhihirikia kwa karibu ambacho kinaelezea mfumo wa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 40
  • Imechapishwa: 18/05/2021