Marejeo kuhusu namna ya kuhiji kwa mujibu wa Ibn ´Uthaymiyn

Swali: Ni marejeo yepi mazuri kwa anayetaka kujua sifa ya Hajj na ´Umrah?

Jibu: Tungo zilizotungwa na wanachuoni waaminifu kuhusu namna ya kutekeleza ´ibaadah ya hajj na ´Umrah ni nyingi. Hadiyth iliyokusanya kuhusu namna ya hajj ni ile ya Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh). Hakika ametaja namna ya sifa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuanzia alipotoka al-Madiynah mpaka ile siku ya ´Iyd kwa upambanuzi. Hakika ni Hadiyth imekuja kwa njia ya jumla lakini imekusanya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1414
  • Imechapishwa: 20/12/2019