Swali: Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yote yataingia Motoni.”

Je, hii ni dalili ya ukafiri wa mapote haya au ni matishio tu?

Jibu: Yote yataingia Motoni kama jinsi alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hazungumzi kwa matamanio yake. Lakini kuko ambao wataingia Motoni kwa kufuru yao na watadumishwa humo milele na kuna ambao wataingia Motoni kwa dhambi zao na maasi yao makubwa, lakini hawa hawatodumishwa humo milele ikiwa maasi yao na uhalifu wao hauwatoi kwenye Dini. Kuna uwezekano akaadhibiwa Motoni lakini likibidi hilo hatodumishwa humo milele. Ni lazima kupatikane ufafanuzi huu. Wataingia Motoni ima ni kwa sababu ni makafiri au ni kwa sababu ni watu wa madhambi makubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_03.mp3
  • Imechapishwa: 31/05/2015