Mapokezi kwamba Moto utamalizika hayakusihi

Swali: Ni upi usahihi wa yale yanayopokelewa kutoka kwa baadhi ya Salaf juu ya masuala ya kumalizika kwa Moto? Je, hayo yametajwa juu ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah?

Jibu: Haya yametajwa na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika “Haadiy Arwaah”. Ametaja mapokezi kutoka kwa baadhi ya Salaf ambao ni Maswahabah na wengineo kwamba Moto utamalizika. Lakini mapokezi haya mengi yayo hayakusihi. Cheni za wapokezi wake zimekatika. Maoni ya sawa ni kwamba Pepo na Moto vitadumu milele na havitomalizika na kuteketea. Maandiko ndani ya Qur-aan na Sunnah yanajulisha hivo. Baadhi ya wanazuoni wamefasiri maoni hayo kwamba kitachomalizika ni lile tabaka ambalo watakuwemo ndani yake waislamu watenda maasi. Kuhusu Moto wa makafiri hautomalizika.

Shaykh-ul-Islaam [Ibn Taymiyyah] haonelei kuwa Moto utamalizika. Bali yeye anaona kuwa utabaki. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja maoni ya pande zote mbili na akarefusha katika “Shifaa´-ul-´Aliyl” na kwenginepo. Kinachofahamika ni kwamba yeye anaonelea maoni haya. Pengine anayo maoni mawili ambapo amerejea katika moja kati ya mawili hayo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 07/08/2021