Mapito ya Ibn ´Uthaymiyn juu ya ´Aswr kwamba ni zama


Swali: Allaah ameapa kwa dhuhaa, akaapa kwa alfajiri na akaapa kwa usiku. Ni kwa nini alasiri hapa iwe na maana ya zama? Je, kuna karina inayofahamisha hivo?

Jibu: Karina inayoonyesha kuwa makusudio ya alasiri  ni zama ni kwa kuwa Allaah (Ta´ala) ametaja kile anachokiapia – ambayo ni yale matendo ya waja – ambayo yanakuwa katika alasiri hii:

وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

“Naapa kwa al-‘Aswr. Hakika ya mwanadamu bila shaka yumo katika khasara, isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana kwa haki na wakausiana subira.” (al-´Aswr 103:01-03)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/818
  • Imechapishwa: 22/05/2020