Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini mwenye nguvu anapendwa zaidi na Allaah kuliko muumini dhaifu – na kwa wote wawili kuna kheri.”[1]

Hadiyth inathibitisha mapenzi kwa Allaah na kwamba yamefungamana na kile Anachokipenda na yule anayefanya yale yanayoyasababisha. Vilevile inafahamisha kuwa yamefungamana na matakwa na utashi Wake. Vilevie inaonyesha kuwa mapenzi Yake yanatofautiana; kumpenda Kwake muumini mwenye imani yenye nguvu ni kukubwa kuliko anavyompenda muumini mwenye imani dhaifu.

[1] Muslim (2664), Ibn Maajah (79) na Ahmad (8611).

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjatu Quluub-il-Abraar, uk. 35
  • Imechapishwa: 27/02/2019