Kupenda ni Sifa miongoni mwa Sifa za Allaah ambayo Ahl-us-Sunnah wanamthibitishia nayo kwa njia inayolingana na utukufu na ukubwa wa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Kumekuja dalili zake katika Qur-aan katika Aayah nyingi. Vilevile katika Sunnah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) anapenda kama jinsi inavyolingana na utukufu na ukubwa Wake. Anapenda na sio kwa sababu Anamuhitajia yule Anayempenda. Bali anafanya hivo kwa kufurahia ule wema wa yule anayempenda. Mapenzi Yake (Jalla wa ´Alaa) ni ya ukamilifu na sio kwa sababu ya haja. Bali ni mapenzi yaliyojitosheleza. Anampenda mja Wake kwa mja kujikurubisha Kwake. Mapenzi Yake (Jalla wa ´Alaa) kwa mja Wake ni miongoni mwa matunda kwa kuwa pamoja na mja wake kwa aina maalum.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 437
  • Imechapishwa: 13/05/2020