Mapendekezo ya al-Waadi´iy kwa al-Hajuuriy

Wale walio na wanachuoni Da´wah yao ni moja. Yeye (al-Hajuuriy) hastahiki kwa mujibu wa wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah mpaka atubu kwa Allaah. Pale atapotubu kwa Allaah kwa tawbah ilioeneza masharti yake, mwenye kutubu Allaah humsamehe. Ama kuendelea kuwatukana wanachuoni, kuwadharau, kuwachezea shere, kusema kuwa ni wapotevu na anajitambua yeye mwenyewe tu, anajidhuru yeye mwenyewe na anaidhuru Dammaaj ambayo ni sehemu ya Shaykh Muqbil (Rahimahu Allaah).

Shaykh Muqbil (Rahimahu Allaah) alifanya Ijtihaad, lakini sio kila mwenye kufanya Ijtihaad anapatia. Mwanachuoni akifanya Ijtihaad akapatia, anapata ujira mara mbili, na akifanya Ijtihaad na akakosea, anapata ujira mara moja. Alifanya Ijtihaad kwake lakini hakuna mwanaadamu aliyesalimika na kukosea. Vinginevyo ni kuwa al-Hajuuriy hastahiki kufunza hata wanafuzni watano. Atakuja kuwafunza mfumo wake. Watoto wa waislamu ni amana. Haifai kuwafunza kitu kinachoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2865
  • Imechapishwa: 18/01/2017