Swali: Mume ana haki ya kuchukua mapato ya mke?

Jibu: Hili lina uhusiano na mume pindi alipooana naye. Hakumuoa isipokuwa baada ya yeye kuajiriwa katika kazi yake? Au alianza kufanya kazi baada ya kuoana? Je, walikubaliana kabla au baada ya ndoa kugawa mapato na kusaidiana kwa hilo? Ikiwa kulikuwa kitu kuhusu mapatano, ni lazima yatimizwe. Hata hivyo ikiwa hakuna kitu kama hicho, mume hana haki yoyote ya kuchukua sehemu katika mapote yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (238)
  • Imechapishwa: 20/09/2020