Mapambo na picha aina ya kipepeo


Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa pambo la dhahabu aina ya kipepeo, wembe au moyo? Je, haya ni haramu? Mmoja katika waalimu wa kike wanasema kuwa haya ni shirki?

Jibu: Pambo la dhahabu kikiwa ni cha aina ya mnyama hakijuzu. Kwa sababu kuvaa picha ni haramu. pasi na kujali picha hiyo imetengenezwa, kama pambo la dhahabu kama ilivyokuja katika swali hili, au vipepeo vilivyochorwa, watu au viumbe vengine vilivyoumbwa, vinavokuwa kwenye sweta au vitambara vyengine. Zote hizi ni haramu. Kutumia kitu chenye picha au picha yenyewe ni haramu.

Isipokuwa picha ilioko kwenye kitu kinachodhalilishwa kama mfano wa picha zilizoko kwenye magodoro, mito na mfano wake. Kwa mujibu wa maoni sahihi kwamba inafaa kuzitumia na haina neno.

Kuhusu maneno ya mwalimu wa kike kwamba ni shirki, sio shirki. Hata hivyo ni haramu.

Swali: Vipi ikiwa pambo la dhahabu hilo ni kwa aina ya wembe?

Jibu: Haina neno ijapo mimi ni mwenye kulichukia hilo kutokana na kwamba kimefungamana na mwanamke kunyoa jinsia yake au mfano wa hayo. Haitakiwi kwa mwanamke kujipamba na kila kitu ambacho kimefungamana na mambo haya.

  • Mhusika: Imam Muhammad bin Sâlih bin ´Uthaymîn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (46 A)
  • Imechapishwa: 24/06/2021